0







Simu nyingi za kisasa huja na programu ya kucheza muziki. Programu hii hutosha kwa mambo mengi ya msingi ya kucheza mziki na kuipangilia. Lakini vipi kama unahitaji muonekano tofauti na mambo matamu zaidi kama kucheza muziki unapochomeka hedifoni na kupata picha za wanamuziki sanjari na nyimbo zao?

Tunachambua appu 5 za aina hii kwenye Androidi.

Rocket Player


Ni rahisi sana kuanguka kimapenzi na muonekano wa Rocket Player. Ukiifungua, nyimbo na picha zake hupangiliwa kwa umaridadi sana. Ni rahisi kusogeza skrini juu-chini na pembeni kutafuta nyimbo. Cha kufurahisha zaidi ni kwamba ukichomeka tu hedifoni, Rocket Player inaanza kucheza muziki. Hii inasaidia sana. Chukua picha kama uko kwenye jua kali na hauoni skrini au hautaki kufungua skrini. Appu hii ina skrini yake inayotokea kabla ya kuifungua simu kukupa urahisi wa kubadili nyimbo haraka. Ukifuatilia mipangilio kwa umakini na kupambana na kiingereza kidogo, utaweza kubadili muonekano wa Rocket player kwa kuipa rangi unayotaka, kulazimisha nyimbo zianze kucheza kwa sauti ya kiwango unachotaka unapochomeka hedifoni na kulipia huduma zaidi kama za kutumia hifadhi-pepe (cloud) na kushusha picha za wanamuziki. Unaweza pia kuangalia video au kuchagua kuzificha kwenye Rocket Player.

Shuttle Player

Shuttle Player ni appu inayofanana sana na Google Play Music Player inayopatikana kwenye simu nyingi za Androidi. Sifa kubwa ya appu hii ni uwezo wa kushusha picha za wanamuziki bure kwenye kitumi chako ili zionekane pale unapocheza muziki. Kama Rocket Player, Shuttle inaweza kucheza muziki unapochomeka hedifoni ila huduma hii inawezekana pale unapoingia kwenye mipangilio na kuiwezesha. Jambo lingine la kipekee kwa appu hii ni uwezo wa kutuma nyimbo kwa urahisi kwenda kwa mtu mwingine. Zaidi ya huduma hizo, Shuttle ni rahisi kuielewa na kutumia. Ina mpangilio wa kuridhisha unaorahisisha kutafuta nymbo kirahisi na inatumia rasilimali za simu kidogo kulinganisha na appu pinzani.
aePlayer
9702b3a908fef58d1362947a67e34456_screen_384x640aePlayer inakuweka karibu zaidi na nyimbo unazozipenda. Kinachofanyika ni wewe kuiambia kuwa unapenda nyimbo flani kwa kubonyeza kialama cha moyo juu ya nyimbo zinazocheza na yenyewe itakupa orodha ya nyimbo hizo punde unapoifungua app hiyo. Pili, inakupa orodha ya nyimbo ulizoziweka muda si mrefu uliopita. Zaidi ya hapo, aePlayer ina uwezo wa kushusha picha za wasanii na kuziambatanisha na nyimbo zako pale zinapocheza.

DoubleTwist

Kama unapenda muonekano wa kuvutia, Double Twist ni kwa ajili yako. vigumu kupata appu nyingine iliyo na muonekano maridadi na usio mzito kama wa appu hii. Kwa DoubleTwist unaweza kusikiliza vipindi na redio za ughaibuni na kubadili muziki punde unpowasha skrini bila kuifungua (Lockscreen control). Jambo lingine linaoiweka DoubleTwist mbele ni urahisi wa kuwashirikisha marafiki wa facebook na Twitter kuhusu nini unakisikiliza kiurahisi. App hii inajiunga moja-kwa-moja na facebook ukiiruhusu. DoubleTwist inapambanisha na Rocket Player kwa uzuri ila Rocket player inatisha zaidi kwa uwezo wa kuweza kucheza muziki ukichomeka hedifoni.doubletwist
musiXmatch Player
Musixmatch ni baba lao ikija kwenye appu za muziki kwenye Androidi. Appu hii inakuonesha maneno ya nyimbo(lyrics) za nyimbo, unaweza kujisikiliza wakati unaimba nyimbo na untaweza kugundua nyimbo ambazo huzifahamu kwa kuisikilizisha simu nyimbo hiyo. Pamoja na hayo, unaweza kuipangilia simu kucheza au kusimamisha muziki punde unapochomeka au kutoa hedifoni na kubadili nyimbo bila kufungua simu. Thadhari pekee ni kwamba musixMatch inaweza ikawa nzito kwenye simu yako na kwa sababu hiyo, unaweza usiifurahie kama simu yako ni ya uwezo mdogo au kawaida.
Rocket, Shuttle, aePlayer, Doubletwst na musixMatch ni baadhi tu ya chaguo letu la appu 5 bomba kwa muziki kwenye simu na tableti za Androidi. Nyingine ya kuangalia ni n7 yenye muonekano ambao ni tofauti sana,mediaMonkey na VLC ambazo bado zinafanyiwa matengenezo na zitabadilika kila mara na nyingine nyingi ambazo kila moja ina sifa zake.






chanzo:tk

Post a Comment

YOUR COMMENTS

 
Top