Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema kuwa watu 36 wameuawa katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
![]() |
Basi lililoshambuliwa huko Mandera nchini Kenya. |
Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi hilo amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa Kenya.
Washambuliaji hao walitumia magruneti na
silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio
hilo.
Post a Comment
YOUR COMMENTS