0


Huduma ya ujumbe mfupi wa pupa, WhatsApp umeendelea kupata maboresho baada ya hii. Sasisho hili la sasa linakuwezesha kujua nani katika kundi kaona ujumbe ulioutuma kwa kushikilia ujumbe uliotuma na kubofya kitufe cha taarifa kama inavyooneshwa kwenye picha hapa chini.

 Habari za waliopokea na kusoma Ujumbe wa Kundi,




 ikionesha pia idadi ya watu ambao bado hawajasoma
 ujumbe.
Taarifa zinazoonekana ni pamoja na ujumbe uliotumwa, orodha ya wanakundi waliosoma ujumbe na idadi ya namba zilizosalia kusoma ujumbe huo.

Katika siku za hivi karibuni, WhatsApp inaendelea kubadilisha vile tunavyozungumza ki-teknolojia kwa kujaribu kuweka mambo wazi zaidi. Wengi wanaona kwamba suala hili linazidi kumong’onyoa fragha na kuna uwezekano kukawa na ahueni kwao katika siku za karibuni ila kwa sasa, roho yako inaweza kutulia kujua kwamba WhatsApp wamedhibiti mtu mwingine kuona ujumbe wako umesomwa na watu wangapi kwenye kundi lenu – labda ili kukuepushia aibu kama watu wana tabia ya kupotezea!
WhatsApp inajuaje kwamba wanakundi wamesoma ujumbe?
Kutokana na WhatsApp wenyewe, kama meseji yako imetumwa na kufika kwenye ‘server’ zao (Kompyuta maalumu kwa makampuni), tiki moja itatokea kwako; Kama ujumbe umefika kwenye simu ya muhusika na hata bila ya yeye kuifungua, basi utaona tiki mbili za rangi ya majivu na hizo tiki zitabadilika kuwa za bluu pale mtu wako atakapofungua meseji hiyo. Basi, kwa maelezo hayo,

utaelewa kwamba sio lazima kwamba meseji yako imesomwa na wanakundi bali ni miongoni mwa zile zilizopitiwa kuelekea meseji ya mwisho kupokelewa na msomaji. WhatsApp wanaendelea kusema kwamba, kama watu wakitokea kusoma ujumbe wako, basi utapata alama za bluu.




Chanzo: tecknokona

Post a Comment

YOUR COMMENTS

 
Top